Skip to content

Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".

«كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى».

Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba umma wake wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa!. Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- wakasema: Ni nani atakaye kataa ewe Mjumbe wa Allah?! Akawajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa atakayejisalimisha na akafuata na akamtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ataingia peponi, na ama atakaye asi na akawa hakujisalimisha katika sheria atakuwa kakataa mwenyewe kuingia peponi kwa sababu ya matendo yake mabaya.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Nikuwa kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi kwake ni sehemu ya kumuasi Mwenyezi Mungu.

Kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hupelekea kuipata pepo, na kumuasi kwake kunapelekea kuingia motoni.

Habari njema kwa watiifu walioko katika umma huu, nakuwa wote wataingia peponi isipokuwa atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa umma wake, na pupa yake katika kuwaongoa.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (9/ 92) (7280).

Zaidi (14)

فيض القدير شرح الجامع الصغير.

للمناوي.

المكتبة التجارية الكبرى – مصر.

الطبعة: الأولى.

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين لسليم الهلالي.

ط1.

دار ابن الجوزي.

الدمام.

1415هـ.

التيسير بشرح الجامع الصغير.

للمناوي.

مكتبة الإمام الشافعي.

الرياض.

ط3.