Skip to content
النِّسَاء /

Aya 86

4 : 86

Aya 86 of النِّسَاء (4 : 86). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 86

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٖ فَحَيُّواْ بِأَحۡسَنَ مِنۡهَآ أَوۡ رُدُّوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَسِيبًا

Na mnapo amkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Akikuamkieni mtu yeyote kwa maamkio ya salamu, au dua, au ya namna yoyote ya hishima, au namna nyengine yoyote ile, basi mjibuni kwa maamkio yaliyo mazuri zaidi, au kwa uchache mjibuni kama alivyo kuamkieni yeye. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kutia hisabuni kila kitu, kikubwa na kidogo.