Skip to content
Orodha ya Sura /

الفَاتِحة

الفَاتِحة is chapter 1 of the Quran and has 7 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

7 Aya Sura Na. 1
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU .

Explanation & meanings · 1
  1. Sura inaanza kwa Jina la Mwenyezi Mungu ambaye hapana anayefaa kuabudiwa ila Yeye aliye sifika kwa kila sifa za ukamilifu, na ametakasika na kila la upungufu. Yeye ndiye Mwenye rehema ambaye ananeemesha kwa neema kubwa na ndogo, na za kuwapa wote, na za kuwapa walio khusika. Na Yeye ndiye mwenye kusifika kwa sifa ya Rehema yenye kudumu. (Kauli ya mwanzo aliyo semezwa Mtume s.a.w. na kuamrishwa na Mwenyezi Mungu ni "Iqra` bismi Rabbika", yaani: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi!" Naye Mtume s.a.w. amesema: "Jambo lolote lisilo anziwa kwa Bismillahi ni pungufu." Kila Sura ya Qur'ani, isipo kuwa Sura Attawba, imeanziwa kwa Bismillahi Rrahmani Rrahim.)

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;

Explanation & meanings · 1
  1. Sifa njema za namna yote na katika kila hali ni za Mwenyezi Mungu pekee. Na tunamsifu Yeye kwa sifa zote kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuviumba viumbe vyote na mwenye kuviangalia na kuvilea. (Neno Rabb, kwa Kiarabu, lina maana ya Ubwana na Ulezi na Utengenezaji. Ndiyo tukatumia Mola Mlezi. Neno Baba lina upungufu.)

ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;

Explanation & meanings · 1
  1. Na Yeye ndiye Mwenye rehema ya kudumu, na rehema inatokana naye. Ananeemesha kwa neema zote ndogo na kubwa. (Arrahman ni jina lake Mwenyezi Mungu tu, na hafai mtu kuitwa hivyo.)

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Mwenye kumiliki siku ya malipo.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye kumiliki Siku ya Malipo na Hisabu, yaani Siku ya Kiyama, anafanya atakavyo wala hapana mwenye kushirikiana naye walau kwa kuonekana tu.

إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ

Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada.

Explanation & meanings · 1
  1. Hatumuabudu yeyote ila Wewe tu, wala hatutaki msaada kwa yeyote ila kwako tu.