Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 6 kati ya 839

Ondoa vichujio
Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".
Sahihi Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
"Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
"Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Yakwamba yeye alikuwa akisema anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa" Na anaposhinda jioni anasema: "Kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa, na kwako tutafufuliwa" Akasema: Na mara nyingine: "Na kwako ndio marejeo".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah
Ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku moja alitoka kwake asubuhi pindi alipo sali sala ya asubuhi, na yeye akiwa katika sehemu yake ya kusalia, kisha akarudi baada ya kuingia wakati wa dhuha, naye akiwa amekaa, akasema: "Bado upo kwenye hali yako niliyo kuacha nayo?" Akasema: "Ndio", Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito: Sub-haana llahi Wabihamdihi, Adada khalqihi, Waridhwaa nafsihi, Wazinata Arshihi, Wamidaada kalimaatihi" (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake, kwa idadi ya viumbe vyake, na ridhaa ya nafsi yake, na uzito wa Arshi yake, na wino wa maneno yake)
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake