Skip to content

Amelaaniwa mwenye kumuingilia mke wake kinyume na maumbile

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:

"Amelaaniwa mwenye kumuingilia mke wake kinyume na maumbile".

«مَلْعُون مَنْ أتَى امرأتَه في دُبُرِها».

Imepokelewa naAbu Daud na Nasai katika Sunan Alkubra na Ahmad
Ni nzuri (Hasan)
Ufafanuzi

Anamtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume kumuingilia mkewe katika utupu wake wa nyuma; kuwa amelaaniwa na amefukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.

Katika Faida za Hadithi

Uharamu wa kuwaingilia nyuma wanawake.

Kustarehe na mke sehemu yoyote katika mwili wake isiyokuwa nyuma inafaa.

Muislamu anamuingilia mwanamke katika tupu yake ya mbele kama alivyomuamrisha Mwenyezi Mungu; na ama kwa nyuma kuna kuharibu maumbile, na kupoteza kizazi, na kwenda kinyume na asili salama ya viumbe hai, na kuna madhara makubwa kati ya wanandoa.

Rejea

Sunanu Abii Daud (3/ 489) (2162).

Sunan Alkubraa cha Imam Nasai (8/ 200) (8966).

Musnad wa Ahmad (15/ 457) (9733).

Zaidi (8)

نيل الأوطار.

للشوكاني (6/ 237).

سبل السلام.

للصنعاني (2/ 202).

توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام.

للبسام (5/ 346).

فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام.

لابن عثيمين (4/ 535).