Skip to content
يُونس /

Aya 18

10 : 18

Aya 18 of يُونس (10 : 18). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 18

وَيَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡ وَيَقُولُونَ هَٰٓؤُلَآءِ شُفَعَٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِۚ قُلۡ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعۡلَمُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha,na wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Sema: Je! Mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa Taa'la! Ametakasika na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hawa washirikina wanao mzulia Mwenyezi Mungu kuwa ana washirika, wanaabudu masanamu ya upotovu. Hayawadhuru wala hayawanufaishi. Na wanasema: Masanamu haya yatatuombea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Akhera! Ewe Mtume! Waambie: Hivyo nyinyi mnamwambia Mwenyezi Mungu kuwa ana washirika ambao hawajui, la katika mbingu wala katika ardhi? Mwenyezi Mungu ametakasika na kuwa na washirika, na yote mnayo zua kwa kuwaabudu hao washirika.