Skip to content
الحُجُرَات /

Aya 17

49 : 17

Aya 17 of الحُجُرَات (49 : 17). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الحُجُرَات Aya 18
Sura · الحُجُرَات
Kiswahili · Barawani
49 : 17

يَمُنُّونَ عَلَيۡكَ أَنۡ أَسۡلَمُواْۖ قُل لَّا تَمُنُّواْ عَلَيَّ إِسۡلَٰمَكُمۖ بَلِ ٱللَّهُ يَمُنُّ عَلَيۡكُمۡ أَنۡ هَدَىٰكُمۡ لِلۡإِيمَٰنِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyieni hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.

Explanation & meanings · 1
  1. Wanaona kuwa kusilimu kwao ni kukuunga mkono wewe, Muhammad, na hivyo inastahiki wewe uwashukuru. Sema: Msinisimbulie kusilimu kwenu; kwani kheri yake mnaipata nyinyi. Bali ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye kufanyieni ihsani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli katika hayo madai yenu.