Skip to content
الحُجُرَات /

Aya 10

49 : 10
الحُجُرَات Aya 18
Sura · الحُجُرَات
Kiswahili · Barawani
49 : 10

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ إِخۡوَةٞ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَ أَخَوَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wote wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni ndugu, Imani imezifanya nyoyo zao pamoja. Basi patanisheni baina ya ndugu zenu kwa kufuata udugu wa Imani. Na jiwekeeni nafsi zenu kinga cha kukinga adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kufuata amri yake, na kuepuka anayo yakataza, na huku mkitaraji Mwenyezi Mungu akurehemuni kwa uchamngu wenu.