Skip to content
Orodha ya Sura /

سَبإ

سَبإ is chapter 34 of the Quran and has 54 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

54 Aya Sura Na. 34
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُ فِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote viliomo mbnguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni Mwenye hikima, Mwenye khabari.

Explanation & meanings · 1
  1. Sifa zote nzuri ni haki ya Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Mwenye kuumba, na Mwenye kumiliki, na Mwenye kupanga vyote vilioko mbinguni, na vilioko katika ardhi. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye sifa Akhera, kwa kutamalaki kwake kuliko enea. Naye ndiye Mwenye hikima asiye kosa, Mwenye khabari zote, hapana asicho kijua siri yake.

يَعۡلَمُ مَا يَلِجُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا يَخۡرُجُ مِنۡهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعۡرُجُ فِيهَاۚ وَهُوَ ٱلرَّحِيمُ ٱلۡغَفُورُ

Anajua yanayo ingia katika ardhi na yanayo toka humo, na yanayo teremka kutoka mbinguni, na yanayo panda huko. Na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe.

Explanation & meanings · 1
  1. Anajua kila kinacho ingia katika sehemu za ardhi, kama maji, na khazina, na vilio zikwa, na sehemu za maiti; na kila kinacho toka, kama wanyama, na mimea, na maadeni, na maji ya visima, na chemchem. Na anajua vinavyo teremka kutoka mbinguni, kama Malaika, na Vitabu wanavyo vipokea Manabii, na mvua, na radi; na anajua vinavyo panda ndani yake na kwendea huko, kama Malaika, na a'mali za ibada, na roho. Na Yeye ni Mwingi wa rehema, Mkubwa wa kusamehe.

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَأۡتِينَا ٱلسَّاعَةُۖ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأۡتِيَنَّكُمۡ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِۖ لَا يَعۡزُبُ عَنۡهُ مِثۡقَالُ ذَرَّةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَآ أَصۡغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرُ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ

Na walisema walio kufuru: Haitatufikia Saa (ya Kiyama). Sema: Kwani? Hapana shaka itakufikieni, naapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinacho fichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi; ila vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wenye kukufuru wakasema: Haitujii Saa iliyo ahidiwa kuwa ni ya kufufuliwa na kukusanywa watu. Waambie ewe Mtume! Hapana shaka itakujieni, nami naapa kwa Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya siri, ambaye hapana chenye kughibu na ujuzi wake hata ingawa kiasi ya chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi. Wala kilicho kidogo kuliko chembe, wala kikubwa kuliko hivyo hakikosi kuandikwa katika Kitabu kilicho timia, chenye kubainisha kila kitu. Dharra , tuliyo ifasiri "Chembe", na kisayansi ni Atom kwa hakika katika lugha ya Kiarabu ni kitu kidogo sana, kama sisimizi mdogo, au chembe ya vumbi. Na uzito wa Dharra maana yake ni uzani wake. Na Aya inaonyesha kuwa kipo kilicho kuwa ni kidogo kuliko Dharra. Na yafaa kutaja hapa kuwa sayansi za sasa zimethibitisha kuwa Dharra, yaani Atom, imegawika katika sehemu ndogo zaidi nazo ni Nucleus na Electrons. Na haya haya hayakuthibitika ila katika karne ya ishirini ya kuzaliwa Nabii Isa.

لِّيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ

Ili awalipe walio amini na wakatenda mema. Hao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ili Mwenyezi Mungu awathibitishe walio amini na wakatenda mema kwa ajili ya nafsi zao na kwa ajili ya watu wengine. Hao Waumini watendaji watapata kwa Mwenyezi Mungu msamaha wa kuwafutia madhambi yao, na riziki kunjufu isiyo na masimbulizi ndani yake.

وَٱلَّذِينَ سَعَوۡ فِيٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٞ مِّن رِّجۡزٍ أَلِيمٞ

Na wale walio jitahidi kuzipinga Ishara zetu wakaona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hao walio zishughulisha nafsi zao kuipiga vita Qur'ani kutaka kuishinda amri ya Mwenyezi Mungu katika kumsaidia Mtume wake, hao watapata adhabu katika adhabu za mwisho wa ubaya na uchungu.