34 : 26
قُلۡ يَجۡمَعُ بَيۡنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفۡتَحُ بَيۡنَنَا بِٱلۡحَقِّ وَهُوَ ٱلۡفَتَّاحُ ٱلۡعَلِيمُ
Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu Mwenye kujua.
Explanation & meanings · 1
- Waambie: Mola wetu Mlezi atatukusanya Siku ya Kiyama, kisha atatuhukumu kwa haki. Na Yeye Subhanahu ndiye Hakimu wa kila shauri, Mwenye kujua kwa hakika yetu sisi na yenu nyinyi.