34 : 48
قُلۡ إِنَّ رَبِّي يَقۡذِفُ بِٱلۡحَقِّ عَلَّٰمُ ٱلۡغُيُوبِ
Sema: Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa Haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema yaliyo ghaibu.
Explanation & meanings · 1
- Waambie: Hakika Mola wangu Mlezi huitupa Haki juu ya baat'ili (uwongo) ikauondoa. Na Yeye ndiye Mwenye kuijua vyema ghaibu; hapana siri inayo fichikana kwake.