34 : 44
وَمَآ ءَاتَيۡنَٰهُم مِّن كُتُبٖ يَدۡرُسُونَهَاۖ وَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهِمۡ قَبۡلَكَ مِن نَّذِيرٖ
Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia Mwonyaji kabla yako wewe.
Explanation & meanings · 1
- Na Mwenyezi Mungu hakuwateremshia Waarabu Vitabu vya mbinguni wavisome; wala hutukupata kuwapelekea Mwonyaji kabla yako wa kuwahadharisha na matokeo ya ukafiri wao.