Skip to content
Orodha ya Sura /

الفَلَق

الفَلَق is chapter 113 of the Quran and has 5 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

5 Aya Sura Na. 113
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ

Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko,

Explanation & meanings · 1
  1. Sema najikinga na Mola Mlezi wa asubuhi inapo pambazuka kutokana na usiku.

مِن شَرِّ مَا خَلَقَ

Na shari ya alivyo viumba,

Explanation & meanings · 1
  1. Na shari ya kila chenye shari katika viumbe, ambavyo hapana wa kuzuia shari yao ila Mwenye kumiliki amri yao.

وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ

Na shari ya giza la usiku liingiapo,

Explanation & meanings · 1
  1. Na shari ya usiku unapo kuwa totoro.

وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّٰثَٰتِ فِي ٱلۡعُقَدِ

Na shari ya wanao pulizia mafundoni,

Explanation & meanings · 1
  1. Na shari ya anaye pita baina ya watu kwa sababu ya kuwafisidi.

وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ

Na shari ya hasidi anapo husudu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na shari ya hasidi anaye tamani iondoke neema kwa wengine.