Skip to content

Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:

"Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake".

«أَسْوَأُ النَّاسِ سَرَقَةً الَّذِي يَسْرِقُ صَلَاتَهُ» قَالَ: وَكَيْفَ يَسْرِقُ صَلَاتَهُ؟ قال: «لَا يُتِمُّ رُكُوعَهَا، وَلَا سُجُودَهَا».

Imepokelewa na Ibnu Hiban
Sahihi
Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwizi mbaya zaidi kuliko wote ni yule anayeiba swala yake; na hii ni kwakuwa; kuchukua mali ya mtu mwingine huenda mtu akanufaika nayo duniani, tofauti na mwizi huyu, kwa sababu kaiba haki ya nafsi yake katika thawabu na malipo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na vipi mtu anawezaiba kutoka katika swala yake? Akasema: Kwa kutotimiza rukuu zake wala sijida zake; na hii ni pale anapofanya haraka kutoka katika rukuu na sijida, hazileti katika namna ya ukamilifu.

Katika Faida za Hadithi

Umuhimu wa kuifanya vizuri sala, na kuzileta nguzo zake taratibu na kwa utulivu.

Amemsifu mtu asiyetimiza rukuu yake na sijida yake kuwa ni mwizi, ikiwa ni ishara ya kulichukia hilo, na tahadhari juu ya uharamu wake.

Uwajibu wa kutimiza rukuu na sijida ndani ya swala na kutulizana ndani yake.

Rejea

Swahiih Ibni Maajah (5/ 209) (1888).

Zaidi (4)

الشّافي في شرح مسند الشّافعي (1/613).

الكاشف عن حقائق السنن (3/1020).

التنوير (2/373).

نيل الأوطار (2/ 311).