Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 17 kati ya 839

Ondoa vichujio
Anasimulia yakuwa yeye alikuwa akitoa takbira katika swala zote za faradhi na zinginezo, ndani ya ramadhani na nje ya ramadhani, anatoa takbira anaposimama, kisha anatoa takbira wakati anarukuu, kisha anasema: Sami'allaahu liman hamidah, kisha anasema: Rabbanaa walakal hamdu, kabla hajasujudu, kisha anasema: 'Allaahu Akbaru' wakati anapoporomoka kwenda kusujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati anasujudu, kisha anatoa takbira wakati ananyanyua kichwa chake kutoka katika sijida, kisha anatoa takbira wakati ananyanyuka kutoka katika kikao kwenda katika rakaa ya pili, na anafanya hivyo katika rakaa zote, mpaka anamaliza swala, kisha anasema anapomaliza swala: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika shetani amekaa kati yangu na swala yangu na kisomo changu ananichanganya, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu", anasema: Nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akamuondosha kwangu.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Pindi mtakaposwali basi nyoosheni safu zenu, kisha akuongozeni mmoja wenu, atakapotoa takbira basi toeni takbira, na anaposema: "Ghairil maghdhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" [Suratul Fatiha: 7], basi semeni: Aaamiin (Ewe Mola wetu Mlezi tukubalie maombi) Atakujibuni Mwenyezi Mungu, atakapotoa takbira na akarukuu basi nanyi toeni takbira na mrukuu, kwani imamu anatakiwa kurukuu kabla yenu, na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:"Hiyo itakwenda na ile, na akisema: Samia'llaahu liman hamidah, semeni: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, Mwenyezi Mungu anakusikieni, kwani Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- alisema kupitia ulimi wa Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi, na akitoa takbira akasujudu basi sujuduni, kwani imamu anatakiwa asujudu kabla yenu na anyanyuke kabla yenu", akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hiyo inakwenda ile, na akifika mahali pa kukaa basi kauli ya mwanzo ya mmoja wenu iwe ni: Attahiyyatut twayyibaatu as swalawaatu lillaah, assalaam alaika ayyuhan nabiyyu warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu alainaa wa alaa ibaadillaahis swaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega yake anapofungua swala, na anapotoa takbira ya kurukuu, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anainyanyua pia, na akasema: "Sami'a llaahu liman hamidahu" Yaani: Amemsikia Mwenyezi Mungu yule aliyemuhimidi, "Rabbanaa walakal hamdu" Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, na alikuwa hafanyi hivyo katika sijida.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Alinifundisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake, namna ya tashahudi iletwayo ndani ya sala, na kiganja changu kikiwa kati ya viganja vyake, kama anavyonifundisha sura ndani ya Qur'ani: "Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu" Tafsiri yake: Maamkizi (Amani) ni ya Mwenyezi Mungu, na swala na vile vilivyo vizuri, amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, nashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni mjumbe wake. Na katika lafudhi yao nyingine: "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Amani, atakapokaa mmoja wenu katika swala basi na aseme: Attahiyyaatu lillaahi, wasswalawaatu wattwayyibaatu, assalaamu a'laika ayyuhan nabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuh, assalaamu a'lainaa wa a'laa ibaadillaahi sswaalihiin, akisema hivyo, basi dua hii itampata kila mja mwema wa Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini, ash-hadu anlaa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan 'abduhu warasuuluhu, kisha baada ya hapo atachagua maombi yoyote anayotaka kuomba".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia msikitini kisha akaingia mtu mmoja, akaswali, kisha akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akajibu salamu, na akasema: "Rudi kaswali, kwani wewe hujaswali", akarudia kuswali kama alivyoswali mwanzo, kisha akaja, akamsalimia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Rudi kaswali kwani wewe hujaswali" (akafanya hivyo) Mara tatu, akasema: "Namuapa yule aliyekutuma kwa haki, siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivyo, basi naomba nifundishe, akasema: "Utakaposimama katika swala basi toa takbira (sema: Allaahu Akbaru), kisha soma kiasi chepesi ulichonacho katika Qur'ani, kisha rukuu mpaka utulizane ukiwa umerukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane wima, kisha sujudu mpaka utulizane ukiwa umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane ukiwa umekaa, na ufanye hivyo katika swala yako yote".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}.
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim