Tulikuwa pamoja Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana karibu na balehe, tukajifunza imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani, tukaongeza imani kupitia Qur'ani
Imepokelewa kutoka kwa Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Tulikuwa pamoja Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana karibu na balehe, tukajifunza imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani, tukaongeza imani kupitia Qur'ani.
كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِتْيَانٌ حَزَاوِرَةٌ، فَتَعَلَّمْنَا الإِيمَانَ قَبْلَ أَنْ نَتَعَلَّمَ القُرْآنَ، ثُمَّ تَعَلَّمْنَا القُرْآنَ، فَازْدَدْنَا بِهِ إِيمَانًا.
Amesema Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana tuliokaribia kubalehe, wenye nguvu na wakali, tukajifunza kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani; tukazidisha imani kupitia Qur'ani.
Kumebainishwa kuwa imani inazidi na kupungua.
Kupangilia vipaumbele wakati wa kumlea kijana anaekua, na pupa ya kuwajaza imani.
Qur'ani huzidisha imani, na moyo hung'aa kupitia hiyo, na kifua hukunjuka.
Sunanu Ibn Maajah (1/ 42) (61).
Zaidi (2)
مشارق الأنوار الوهاجة ومطالع الأسرار البهاجة في شرح سنن الإمام ابن ماجه (2/ 255).
مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (1/ 227).