Skip to content

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake

Kutoka kwa Waabiswa radhi za Allah ziwe juu yake:

Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.

أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَأَى رَجُلًا صَلَّى وَحْدَهُ خَلْفَ الصَّفِّ، فَأَمَرَهُ أَنْ يُعِيدَ صَلَاتَهُ.

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Ni nzuri (Hasan)
Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja aliyeswali nyuma ya safu peke yake, akamuamrisha arudie swala yake; kwa sababu swala yake haikusihi kwa hali hii.

Katika Faida za Hadithi

Himizo la kuwahi swala ya jamaa na kuwahi mbele kwa ajili yake, na asiswali nyuma ya safu peke yake ili swala yake asiitie katika kubatilika

Amesema bin Hajari: Atakayeanza swala peke yake nyuma ya safu kisha akaingia katika safu kabla ya kunyanyuka kutoka katika rukuu, hatolazimika kurudia, kama ilivyokuja katika hadithi ya Abiibakra, na vinginevyo itakuwa wajibu kwa mujibu wa ujumla wa hadithi ya Waabiswa.

Rejea

Sunanu Abii Daud (2/ 18) (682).

Sunanu Tirmidhiy (1/ 268) (230).

Sunanu Ibn Maajah (2/ 137) (1004).

Musnad wa Ahmad (29/ 524) (18000).

Zaidi (6)

سبل السلام شرح بلوغ المرام.

لمحمد الصنعاني (1/ 378).

توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام.

لعبد الله البسام (2/ 509).

فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام.

لابن عثيمين (2/ 288).