Skip to content

Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja

Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema:

Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja.

تَوَضَّأَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّةً مَرَّةً.

Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja moja, anaosha uso pamoja kusukutua na kupandisha maji puani, na mikono miwili na miguu miwili mara moja moja, na hiki ndicho kiwango cha wajibu.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Kilicho wajibu katika kuosha viungo ni mara moja moja, inayozidi inapendeza kufanya hivyo.

Sheria ya kutia udhu mara moja moja katika baadhi ya nyakati.

Sheria katika kufuta kichwa ni mara moja.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (1/ 43) (157).

Zaidi (1)

إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 244).