Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah)
Kutoka kwa Ka'bu bin Hatim -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah). Atatazama kuliani kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Kisha ataangalia kushotoni kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Na ataangalia mbele yake, na hataona isipokuwa Moto mbele ya uso wake. Basi uepukeni Moto hata kama ni kwa nusu ya tende."
«مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ اللهُ، لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ تُرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلَا يَرَى إِلَّا النَّارَ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ، فَاتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ».
Alieleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa kila Muumini atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama peke yake, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atazungumza naye bila ya muwakilishi, na hakuna mkalimani baina yao wa kutafsiri maneno, hivyo atatazama kulia na kushoto kutokana na hofu kali, labda atapata njia ya kwenda ili aweze kuokolewa na moto uliombele yake. Akitazama upande ulioko kuliani kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mema, na akitazama kushotoni kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mabaya, na akitazama mbele yake hatoona isipokuwa moto, na hatoweza kuukwepa, kwani hakuna budi ni lazima apite juu daraja (Swirat). Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wekeni kinga kati yenu na moto, kama kutoa sadaka na matendo mema, walau kwa kitu kidogo kama nusu ya tende.
Himizo la kutoa sadaka hata kama itakuwa ndogo, na kujipamba na mambo mazuri, na kuamiliana kwa upole na maneno laini.
Ukaribu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake siku ya Kiyama, kiasi kwamba hapatokuwa na kizuizi kati yao, wala muwakilishi wala mkalimani, basi muumini achukue tahadhari asijekwenda kinyume na amri za Mola wake Mlezi.
Ni lazima kwa mtu asidharau anachokitoa sadaka, hata kama ni kidogo, kwani ni kinga ya kutoingia motoni.
Swahiih Al Bukhaariy (9/ 148) (7512).
Swahiih Muslim (2/ 703) (1016).
Zaidi (10)
كنوز رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين.
بهجة الناظرين.
لسليم الهلالي (1/ 476).
نزهة المتقين.
مجموعة من الباحثين (1/ 370).
شرح رياض الصالحين.
لابن عثيمين (2/ 201).
بهجة قلوب الأبرار.
عبد الرحمن آل سعدي (ص181).
Imenukuliwa katika vitabu
11 VitabuZaidi (10)
- العلم الواجب بدون فقه وبدون زيادات1((اِتقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِ تَمْرَة)).
- ترجمة المقاطع المرئية - مشروع هدايات 1(اتقوا النار ولو بشق تمرة)
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 1 «اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشقِّ تَمْرَةٍ».
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 3«مَا مِنْكُم مِنْ أَحَدٍ إلاَ سيُكَلِّمُهُ رَبُّهُ، لَيْس بَيْنَهُ وبَينَهُ تَرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلا يَرَىٰ إلَّا مَا قَدَّمَ، ويَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلا يَرَىٰ إلَّا ما قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلا يَرَى
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 3«اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمرَةٍ».
- مجموعة زاد الحديث(2)1«مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ الله، لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ تُرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَ
- مجموعة زاد الحديث(2)1(ما منكم من أحدٍ)
- مجموعة زاد الحديث(2)1(فاتقوا النَّار ولو بشقِّ تمرة)
- مجموعة زاد الحديث(2)1(مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ اللهُ...)
- مجموعة زاد العقيدة (2)1«مَا مِنْكُمْ أَحَدٌ إِلَّا سَيُكَلِّمُهُ رَبُّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَهُ تُرْجُمَانٌ، فَيَنْظُرُ أَيْمَنَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ مِنْ عَمَلِهِ، وَيَنْظُرُ أَشْأَمَ مِنْهُ فَلَا يَرَى إِلَّا مَا قَدَّمَ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ