Skip to content

Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-:

"Hakika Mwenyezi Mungu hupata wivu, na hakika muumini hupata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia juu yake".

«إِنَّ اللهَ يَغَارُ، وَإِنَّ الْمُؤْمِنَ يَغَارُ، وَغَيْرَةُ اللهِ أَنْ يَأْتِيَ الْمُؤْمِنُ مَا حَرَّمَ عَلَيْهِ».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu hupata wivu na huchukia na hukarahika, kama ambavyo muumini hupata wivu na huchukia na kukarahika, nakuwa sababu ya wivu wa Mwenyezi Mungu ni pale muumini anapoyafanya yale aliyomharamishia Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa machafu kama zinaa liwati (Ushoga na ubasha) wizi na kunywa pombe na mengineyo katika machafu.

Katika Faida za Hadithi

Kutahadhari na hasira na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake pale yanapofanywa maharamisho yake.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (7/ 35) (5223).

Swahiih Muslim (4/ 2114) (2761).

Zaidi (8)

تطريز رياض الصالحين.

لفيصل المبارك (ص62).

شرح رياض الصالحين.

لابن عثيمين (1/ 496).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (1/ 96).

صفات الله عز وجل الواردة في الكتاب والسنة.

لعلوي السَّقَّاف (ص267).