Skip to content
النِّسَاء /

Aya 136

4 : 136

Aya 136 of النِّسَاء (4 : 136). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 136

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِن قَبۡلُۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱللَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا

Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi huyo amekwisha potelea mbali.

Explanation & meanings · 1
  1. Kwa hakika Ujumbe wa mbinguni ni mmoja, kwa kuwa yule Mwenye kutuma ni Mmoja, naye ni Mwenyezi Mungu. Basi enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu na mumsafie niya. Na msadikini Mtume wake Muhammad, na msadiki yaliyo kuja katika Kitabu chake alicho mteremshia, na mtende yaliyo amrishwa humo. Na sadikini Vitabu vilivyo teremshwa kabla yake kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu bila ya mageuzo wala kusahau. Aminini yote hayo. Kwani mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, Muumba wa viumbe vyote, na Malaika, na Mwenye kuyajua yaliyo fichikana, na Vitabu vya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na akaikanusha Siku ya Mwisho, basi huyo ameipotea Njia Iliyo Nyooka, na ametokomea mbali katika njia ya upotovu.