Skip to content
النِّسَاء /

Aya 137

4 : 137

Aya 137 of النِّسَاء (4 : 137). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 137

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ سَبِيلَۢا

Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Imani ni kuit'ii Haki kusio kuwa na ukomo, na kunako endelea daima. Basi wanao taradadi wakababaika si Waumini. Hao ambao wanaamini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakakufuru, na kwa hivyo wakazidi ukafiri wao - Mwenyezi Mungu hatakuwa wa kuwaghufiria watu hao hivyo vitendo vyao viovu, wala hatawaongoa kwenye Haki. Kwani kusamehe kwa Mwenyezi Mungu kunahitajia toba, na kujing'oa na shari, na uwongofu wake ni kwa wale wanao ielekea Haki na wanaitaka.