Skip to content
النِّسَاء /

Aya 101

4 : 101

Aya 101 of النِّسَاء (4 : 101). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 101

وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا

Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.

Explanation & meanings · 1
  1. Swala ni faridha isiyo epukika. Haiachiki Swala kwa ajili ya safari, lakini hana dhambi anaye fupisha Swala safarini. Watokao kwenda safari wakikhofia kuwa makafiri watawaletea ya kuwaudhi, wanaweza kufupisha Swala. Swala za rakaa nne zisaliwe rakaa mbili. Kutahadhari na kuingiliwa na makafiri ni waajibu, kwani wao ni maadui, na uadui wao uwazi.