Skip to content

Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:

Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa, na akasema: "Vitu hivyo havisafishi sawa sawa".

إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُسْتَنْجَى بِرَوْثٍ أَوْ عَظْمٍ، وَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَا تُطَهِّرَانِ».

Imepokelewa na Addar- Alqutni
Sahihi
Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekidhi haja yake sawa iwe haja ndogo au kubwa, kustanji kwa mfupa wa mnyama au kinyesi chake na mabaki yake yaliyokauka; na akasema: Hivyo haviondoshi najisi, na wala havisafishi vizuri.

Katika Faida za Hadithi

Kumebainishwa baadhi ya adabu za kukidhi haja na kustanji.

Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama; kwa sababu: Ima ni najisi, au kwa sababu ni chakula cha wanyama wa Majini.

Katazo la kustanji kwa mfupa; kwa sababu ima ni najisi, au ni chakula cha Majini wenyewe.

Rejea

Sunanu Daaraqutw'niy (1/ 88) (152).

Zaidi (6)

توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام.

لعبد الله البسام (1/ 355).

سبل السلام.

للصنعاني (1/ 118).

مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح.

لعلي القاري (1/ 374).