Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema:
Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi.
مِنَ السُّنَّةِ إِذَا قَالَ الْمُؤَذِّنُ فِي أَذَانِ الْفَجْرِ حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، قَالَ: الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ.
Ameeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa miongoni mwa mambo aliyoyakubali Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sunna zake, ni Muadhini kusema katika Adhana Alfajiri pekee, baada ya kauli yake: "Hayya a'lal falaah" asema: "Asswalaatu khairuni minan nauum" Yaani swala ni bora kuliko usingizi.
Kauli yake: "Katika sunna": Yaani: Sunna ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, inahukumu ya kufikishwa kwa Mtume, yaani inanasibishwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Sunna asema Muadhini katika swala ya Alfajiri baada ya: Hayya a'lal falaah: Aseme: Asswalaatu khairun minan nauum, yaani: Swala ni bora kuliko usingizi, mara mbili; kwa sababu swala ya Alfajiri watu wengi hulala, na wanaamka kwenda katika swala kutoka usingizini, ikahusika swala ya Alfajiri pekee pasina swala nyinginezo.
Swahiih Ibni Khuzeymah (1/ 233) (386).
Sunanu Daaraqutw'niy (1/ 454) (944).
Assunanu Al Kubra cha Bayhaqiy (1/ 623) (1984).
Zaidi (6)
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام.
لعبد الله البسام (1/ 510).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام.
لعبد الله الفوزان (2/ 239).
فتاوى اللجنة الدائمة.
اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء (6/ 62).