Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake
Kutoka kwa Abuu Masoud Al-Answari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika kipandwa changu kimeangamia nakuomba msaada wa usafiri, akasema: "Sina uwezo" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuonyesha kwa mtu atakayeweza kumbeba, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake".
جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: إِنِّي أُبْدِعَ بِي فَاحْمِلْنِي، فَقَالَ: «مَا عِنْدِي»، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَنَا أَدُلُّهُ عَلَى مَنْ يَحْمِلُهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ».
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi kimeangamia kipandwa changu, nipe msaada, na unipe kipandwa kitakachonifikisha, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa udhuru yakuwa yeye hana kitu cha kumsaidia, mtu mmoja akasema na alikuwepo katika mazungumzo: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuelekeza kwa mtu atakaye mbeba, akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atashiriki katika kupata malipo na mtoaji, kwa sababu amemuelekeza muhitaji kwake.
...:
Himizo la kuelekeza katika kheri.
Himizo la kufanya kheri ni katika sababu za kuinyanyua jamii ya kiislamu na kutoshelezana.
Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Hadithi hii ni kanuni kuu, yanaingia hapa matendo yote ya kheri.
Mtu atakaposhindwa kutimiza hitajio la muombaji, basi amuelekeze kwa mwingine.
Swahiih Muslim (3/ 1506) (1893).
Zaidi (5)
شرح النووي على مسلم (11/ 166).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام.
للبسام (7/ 349).
فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام.
لابن عثيمين (6/ 298).
Imenukuliwa katika vitabu
6 Vitabu- UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNAالتحقيق والإيضاح لكثير من مسائل الحج والعمرة والزيارة - النسخة المعتمدة“Mwenye kujulisha katika heri yoyote, basi atapata ujira sawa na mtendaji wake.” ([141])
- YALIYO CHAGULIWA KUTOKA KATIKA SOKO LENYE FAIDA KATIKA THAWABU ZA MATENDO MEMA.المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح"Atakaye julisha juu ya kheri yoyote, atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake".
Zaidi (4)
- الدعوة إلى الله وأخلاق الدعاة«مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ »
- تحفة الأخيار تحفة الأخيار (ببيان جملة نافعة مما ورد في الكتاب والسنة من الأدعية والأذكار)«مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ» [102]
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 1 «مَنْ دَلَّ عَلَىٰ خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ»،
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 2«مَنْ دَلَّ عَلَىٰ خَيْر فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ».