Skip to content
البَقَرَة /

Aya 203

2 : 203

Aya 203 of البَقَرَة (2 : 203). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 203

۞ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ فِيٓ أَيَّامٖ مَّعۡدُودَٰتٖۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوۡمَيۡنِ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۖ لِمَنِ ٱتَّقَىٰۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.

Explanation & meanings · 1
  1. Na mtajeni Mwenyezi Mungu kwa Takbiri na vinginevyo katika siku maalumu, nazo ni siku za kutupa mawe hapo Mina, nazo ni taarikh 11 na 12 na 13. Na si lazima kwa Haji kukaa siku tatu hizi Mina akitupa mawe, bali anaweza kufupiza siku mbili, kwani msimamo wa kheri ni kuchamngu, si idadi. Na daima mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kuwa kwake Yeye mtakusanywa na muulizwe mliyo yatenda. Hayo mawe ni changarawe hutupwa mwahala maalumu katika Mina katika siku ya kuchinja (Idd) na siku tatu zifwatiazo.