Skip to content
Orodha ya Sura /

المَاعُون

المَاعُون is chapter 107 of the Quran and has 7 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

7 Aya Sura Na. 107
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ

Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?

Explanation & meanings · 1
  1. Unamjua anaye kanusha malipo na hisabu ya Akhera?

فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ

Huyo ndiye anaye msukuma yatima,

Explanation & meanings · 1
  1. Ukitaka kumjua basi ni huyo ambaye anaye msukuma yatima kwa nguvu, na anamtumilia mabavu, na anamdhulumu,

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala hahimizi kumlisha masikini.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wala hahimizi kulishwa masikini.

فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ

Basi, ole wao wanao swali,

Explanation & meanings · 1
  1. Maangamio yatawashukia wanao sali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ

Ambao wanapuuza Sala zao;

Explanation & meanings · 1
  1. Maangamio yatawashukia wanao swali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Swala zao wasinafiike nazo.