Skip to content
Orodha ya Sura /

الكَوثر

الكَوثر is chapter 108 of the Quran and has 3 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

3 Aya Sura Na. 108
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِنَّآ أَعۡطَيۡنَٰكَ ٱلۡكَوۡثَرَ

Hakika tumekupa kheri nyingi.

Explanation & meanings · 1
  1. Sisi hakika tumekupa kheri nyingi za daima katika dunia na Akhera.

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنۡحَرۡ

Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.

Explanation & meanings · 1
  1. Ilivyo kuwa umepewa hayo, basi dumisha Swala kwa Mola wako Mlezi kwa usafi kabisa, na uchinje dhabihu wako kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa aliyo kupa ya ukarimu, na akakukhusisha wewe khasa kwa kukupa kheri.

إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ ٱلۡأَبۡتَرُ

Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika huyo anaye kuchukia ndiye aliye katika na kila kheri.