Skip to content
Orodha ya Sura /

التَّكاثُر

التَّكاثُر is chapter 102 of the Quran and has 8 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

8 Aya Sura Na. 102
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ

Kumekushughulisheni kutafuta wingi,

Explanation & meanings · 1
  1. Yamekushughulisheni mkaacha kutimiza yaliyo waajibu na ya ut'iifu kule kujitapa kwenu kwa wana na wafwasi, na kujifakhiri kwa mali, na hisabu, na nasaba, mpaka yakusibuni mauti!

حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ

Mpaka mje makaburini!

Explanation & meanings · 1
  1. Mpaka yakusibuni mauti!

كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Sivyo hivyo! Mtakuja jua!

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika mtakuja jua matokeo ya upumbavu wenu na mapuuza yenu.

ثُمَّ كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!

Explanation & meanings · 1
  1. Na hakika bila ya shaka mtakuja jua natija ya hayo!

كَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ

Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,

Explanation & meanings · 1
  1. Ama kwa hakika lau mngeli jua kwa yakini uovu wa mwisho wenu bila ya shaka mngeli ogopa huko kushindania kurindika mali, na mngeli jitengenezea Akhera yenu.