Skip to content

Zimeteremshwa kwangu aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu, sura mbili za kinga

Imepokelewa kutoka kwa Uqba bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:

"Zimeteremshwa kwangu aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu, sura mbili za kinga"

«أُنْزِلَ -أَوْ أُنْزِلَتْ- عَلَيَّ آيَاتٌ لَمْ يُرَ مِثْلُهُنَّ قَطُّ، الْمُعَوِّذَتَيْنِ».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Ameeleza Ukba bin Aamiri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema kumwambia: Usiku huu Mwenyezi Mungu kaniteremshia aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu -yaani katika kuomba kinga- nazo ni sura mbili za kinga: Suratu (Qul Auudhubirabbil falaq), na suratu (Qul Auudhubirabbin naas).

Katika Faida za Hadithi

Kumebainishwa ukubwa wa fadhila wa sura mbili hizi.

Himizo la kuomba kinga kupitia sura hizi dhidi ya kila shari.

Rejea

Swahiih Muslim (1/ 558) (814).

Sunanu Al Nasaai (2/ 158) (952).

Zaidi (1)

ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (12/ 312).