Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazo swaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
"Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazo swaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka".
«صَلَاةٌ فِي مَسْجِدِي هَذَا خَيْرٌ مِنْ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ إِلَّا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ».
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuswalia katika msikiti wake, nakuwa ni thawabu bora kuliko swala elfu moja (1000) katika misikiti mingine katika misiti ya ardhini, isipokuwa msikiti mtukufu wa Makka, huo ni bora kuliko swala ya msikiti wake rehema na amani ziwe juu yake.
...:
Kuzidishwa kwa malipo ya swala katika msikiti mtukufu (wa Makka), na msikiti wa Mtume.
Swala katika msikiti mtukufu wa Makka ni bora kuliko swala laki moja (100,000) katika misiki mingine.
Swahiih Al Bukhaariy (2/ 60) (1190).
Swahiih Muslim (2/ 1012) (1394).
Zaidi (2)
فتح الباري (3/67).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (24/ 684).
Imenukuliwa katika vitabu
4 Vitabu- UCHAMBUZI NA UFAFANUZI WA MASUALA MENGI YA HIJA, UMRA NA ZIARA KWA MUJIBU WA MUONGOZO WA QUR'ANI NA SUNNAالتحقيق والإيضاح لكثير من مسائل الحج والعمرة والزيارة - النسخة المعتمدة"Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazoswaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka." ([146])
- YALIYO CHAGULIWA KUTOKA KATIKA SOKO LENYE FAIDA KATIKA THAWABU ZA MATENDO MEMA.المنتقى من المتجر الرابح في ثواب العمل الصالح"Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni Bora kuliko Sala elfu moja zinazo Swaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka".
- Fadhila na adabu za Msikiti wa bwana Mtume na hukumu za kuzuru kaburi la Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kaburi za Maswahaba zake wawili, Mwenyezi Mungu awe radhi naoفضائل وآداب المسجد النبوي، وأحكام زيارة قبر النبي عليه الصلاة والسلام وقبري صاحبيه"Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazoswaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka." ([2])