Skip to content

Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake:

Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri.

أن النبي صلى الله عليه وسلم كان لا يَدع أربعا قَبل الظهر وركعتين قبل الغَدَاة.

Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Ufafanuzi

Ameeleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akidumu na swala za sunna ndani ya nyumba yake na wala haziachi: Rakaa nne kwa salamu mbili kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri.

Katika Faida za Hadithi

Sunna ya kuzihifadhi na kudumu na rakaa nne kabla ya swala ya Adhuhuri, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri.

Kilicho bora ni swala za sunna ziswaliwe nyumbani, na ndivyo alivyoeleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (2/ 59) (1182).

Zaidi (2)

توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام.

لعبد الله البسام (2/ 379).