Peaneni zawadi, mtapendana
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- anasema:
"Peaneni zawadi, mtapendana."
«تَهَادَوا تَحَابُّوا».
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza Muislamu kuwa abadilishane zawadi na ndugu yake Muislamu, na kuwa zawadi ni miongoni mwa sababu za mapenzi na kuziunganisha nyoyo.
Ni sunna kutoa zawadi; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameamrisha kufanya hivyo.
Zawadi ni sababu ya kuleta mapenzi.
Inampasa mwanadamu afanye kila ambacho ndani yake kinaleta mapenzi kati yake na watu wengine, sawa sawa iwe ni katika zawadi au kuwa mpole, au katika maneno mazuri au katika ukunjufu wa uso kwa kadiri awezavyo.
Assunanu Al Kubra cha Bayhaqiy (6/ 169).
Zaidi (5)
الأدب المفرد للبخاري (ص:208) (594).
مسند أبي يعلى الموصلي (11/ 9) (6148).
فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام (4/ 319).
فيض القدير (3/ 271).
التيسير بشرح الجامع الصغير (1/ 457).