Skip to content
الأنفَال /

Aya 46

8 : 46

Aya 46 of الأنفَال (8 : 46). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنفَال Aya 75
Sura · الأنفَال
Kiswahili · Barawani
8 : 46

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَنَٰزَعُواْ فَتَفۡشَلُواْ وَتَذۡهَبَ رِيحُكُمۡۖ وَٱصۡبِرُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika mambo mlio amrishwa na mlio katazwa. Na wacheni kuzozana na kukhitalifiana. Hayo ndiyo yanayo pelekea kupoteza nguvu na kushindwa. Na vumilieni mkipata shida za vita. Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanao vumilia wakasubiri kwa kuwapa msaada na kuwaunga mkono, na kuwalipa malipo mema.