Skip to content
المَائدة /

Aya 105

5 : 105

Aya 105 of المَائدة (5 : 105). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 105

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَيۡكُمۡ أَنفُسَكُمۡۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا ٱهۡتَدَيۡتُمۡۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Enyi mlio amini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni walio potoka ikiwa nyinyi mmeongoka. Ni kwa Mwenyezi Mungu ndio marudio yenu nyote; basi atakwambieni yale mliyo kuwa mkiyatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi mlio amini! Fanyeni pupa ya kwendea kwenye matengenezo ya nafsi zenu kwa kumt'ii Mwenyezi Mungu. Upotovu wa mwengineo hautakudhuruni ikiwa nyinyi mmo kwenye uwongofu na mnalingania Haki. Na nyote nyinyi marejeo yenu ni Mwenyezi Mungu peke yake Siku ya Kiyama. Hapo atakupeni khabari ya vitendo vyenu, na kila mmoja wenu atamlipa kwa aliyo yatanguliza, na wala hapana hata mmoja atae shikwa kwa dhambi za mwenginewe.