5 : 104
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ قَالُواْ حَسۡبُنَا مَا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ءَابَآؤُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَهۡتَدُونَ
Na wanapo ambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, na kwa Mtume, husema: Yanatutosha tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka?.
Explanation & meanings · 1
- Na hawa makafiri wakiambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu katika Qur'ani, na aliyo yaeleza Mtume, ili mpate kuongoka kwa kuyafuata, wao husema: Yanatutosha tuliyo wakuta nayo baba zetu. Yawafalia hawa kusema hayo? Ijapo kuwa hao baba zao ni kama nyama hoa, hawajui lolote la haki, wala hawaijui njia ya kuendea yaliyo sahihi.