Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 52 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi Akamwambia: Iangalie hiyo pepo na yale niliyo waandalia humo watu wa peponi, basi Jibrili akaiangalia Pepo kisha akarudi, akasema: Naapa kwa utukufu Wako ewe Mwenyezi Mungu hatozisikia mtu yeyote habari za pepo kisha asiingie humo, kisha akamuamrisha kuizungushia Pepo hiyo mambo yenye kuchukiza, kisha akamwambia nenda tena ukaiangalie na uangalie yale niyowaandalia watu wake humo peponi. Basi akaiangalia ghafla akaiona imezungushwa vyenye kuchukiza, akasema: Naapa kwa utukufu Wako kwa hakika ninahofia kuwa hatoingia mtu yeyote. Akasema kumwambia Jibrili nenda na uuangalie Moto na yale niliyo waandalia humo watu wa Motoni. Basi akauangalia Moto na akauona Moto ulivyopambwa, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu Wako hatoingia yeyote humo, basi akaamrisha ukazungushwa mambo yenye kutamanisha, basi akamwambia: Rudi na uuangalie tena. Basi akauangalia akaukuta umepambwa na kuzungushwa yenye kutamanisha, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu wako kwa hakika nahofia yakuwa hatosalimika mtu yeyote isipokuwa ataingia Motoni."
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
"Kwa hakika mimi nitakuwa kwenye Birika langu namtazama kila mwenye kuja kwangu kunywa, na kuna watu watafukuzwa, na nitasema: Ewe Mola wangu huyu anatokana na mimi na ni katika umma wangu, basi ataambiwa: Hivi unajua waliyoyafanya baada yako? Namuapia Mwenyezi Mungu, hawakuacha kurudi nyuma na kutoka katika dini yao."
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu, kwani mimi nilisikia mkanyago wa viavu vyako mbele yangu huko Peponi" Akasema: Sijawahi kufanya amali yoyote yenye matarajio kwangu isipokuwa sijawahi kutia udhu wowote, katika nyakati za usiku au mchana, isipokuwa ninaswali kwa udhu huo kiasi nilichoandikiwa niswali katika rakaa.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Peponi kuna daraja mia moja baina ya kila daraja mbili ni kama umbali wa mbingu na ardhi, na Firdausi iko daraja ya juu zaidi kuliko zote, na ndani yake ndiko inako chimbuka mito yote minne ya pepo, na juu yake ndiko inakokuwa Arshi, Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi".
Sahihi Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
Alitusimulia Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu vipi kafiri atafufuliwa akitembea kwa uso wake? Akasema: "Hivi yule aliyemfanya atembee kwa miguu miwili hawezi kumfanya atembee kwa uso wake siku ya Kiyama?" Akasema Qatadah: Kwa nini asiweze, ninaapa kwa utukufu wa Mola wetu anaweza kufanya hivyo.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hicho chombo cha Birika kiko vipi? Akasema: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa hakika vyombo vyake ni vingi kama wingi wa nyota mbinguni na sayari zake eleweni vyema kuwa kung'aa kwake kutakuwa katika usiku usio na mwezi, pako safi, vyombo vya peponi atakaye kunywa katika vyombo hivyo hatopatwa na kiu milele wala kiu hakitomrudia, na maji hayo yanaruka na kububujika kupitia mabomba mawili yaliyo juu ya peponi, yeyote atakaye kunywa katika Birika hilo hatopatwa na kiu, upana wake ni sawa na urefu wake ambao ni sawa kutoka Amman mpaka Aila (Ni katika miji ya Jordan, baina yake ni km 330) maji yake ni meupe mno kuliko maziwa, na ni matamu kuliko asali."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake