Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 7 kati ya 839

Ondoa vichujio
Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali Ewe mwanadam lau madhambi yako yangefika mawinguni kisha ukaniomba msamaha ningekusamehe wala sijali Ewe mwanadam, lau ungenijia na thamani ya dhambi za dunia, kisha ukakutana nami bila kunishirikisha na chochote, ningekuletea msamaha ujazo sawa na ardhi".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe", Kisha akasoma aya hii: "Na wale ambao wakifanya machafu au wakizidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha kutokana na madhambi yao" [Al-Imran: 135].
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
"Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
"Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini, na wala msiwauwe watoto wenu, na wala msilete uzushi mtakouzua kwa mikono yenu na miguu yenu, na wala msiasi katika wema, basi atakayeyatimiza hayo miongoni mwenu basi malipo yake yatakuwa juu ya Mwenyezi Mungu, na atakayetenda lolote katika hayo akaadhibiwa katika dunia basi hiyo ndiyo kafara kwake, na atakayetenda lolote katika hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi hilo litabakia kwa Mwenyezi Mungu akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu" Tukampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
"Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Sahihi Imepokelewa na Hakim na Bayhaqy
"Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake."
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim