Skip to content
Orodha ya Sura /

الجُمعَة

الجُمعَة is chapter 62 of the Quran and has 11 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

11 Aya Sura Na. 62
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡمَلِكِ ٱلۡقُدُّوسِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Vitu vyote viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi vinamsabihi na kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa laiki, Yeye ndiye Mfalme wa kila kitu, Mwenye kuendesha atakavyo bila ya mpinzani, Mwenye kutakasika kwa ukamilifu na kila cha upungufu, Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima ya kufika mwisho.

هُوَ ٱلَّذِي بَعَثَ فِي ٱلۡأُمِّيِّـۧنَ رَسُولٗا مِّنۡهُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتِهِۦ وَيُزَكِّيهِمۡ وَيُعَلِّمُهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَإِن كَانُواْ مِن قَبۡلُ لَفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu ndiye aliye mtuma Mtume kwa watu wasio jua kuandika, naye ni katika wao wenyewe, anawasomea Aya zake Mwenyezi Mungu, na anawasafisha na mambo machafu ya itikadi na tabia, na anawafundisha Qur'ani na kuijua Dini. Na wao kabla ya kuletwa yeye walikuwa wamepotoka kabisa kuiacha haki.

وَءَاخَرِينَ مِنۡهُمۡ لَمَّا يَلۡحَقُواْ بِهِمۡۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Na pia Mwenyezi Mungu amempeleka Muhammad kwa watu wenginewe, ambao hawajaja bado, lakini watakuja. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima ya kufikia ukomo katika vitendo vyake.

ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayo mpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Kuletwa Mtume huko ni fadhila inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Anamkirimu kwayo aliye mkhitari katika waja wake. Na Mwenyezi Mungu peke yake, ndiye Mwenye fadhila kubwa.

مَثَلُ ٱلَّذِينَ حُمِّلُواْ ٱلتَّوۡرَىٰةَ ثُمَّ لَمۡ يَحۡمِلُوهَا كَمَثَلِ ٱلۡحِمَارِ يَحۡمِلُ أَسۡفَارَۢاۚ بِئۡسَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anaye beba vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.

Explanation & meanings · 1
  1. Mfano wa Mayahudi walio funzwa Taurati, na wakalazimishwa waifuate, na wao hawakuifuata kwa vitendo, ni mfano wa punda aliye beba vitabu ambavyo hajui ndani yake mna nini. Ni mbaya mno mfano wa watu wanao kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hawasaidii kufikilia uwongofu watu ambao kazi yao ni kudhulumu.