Skip to content
الصَّف /

Aya 6

61 : 6

Aya 6 of الصَّف (61 : 6). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الصَّف Aya 14
Sura · الصَّف
Kiswahili · Barawani
61 : 6

وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٖ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِي ٱسۡمُهُۥٓ أَحۡمَدُۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kumbuka pale Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume nimetumwa kwenu, mwenye kusadikisha yaliyo nitangulia yaliomo katika Taurati, na kukupeni bishara ya Mtume atakaye kuja baada yangu. Jina lake ni Ahmad. Alipo kuja huyo Mtume aliye bashiriwa kwa Ishara zilizo wazi wakasema: Haya uliyo tujia nayo ni uchawi dhaahiri! (Kwa ushahidi wa kubashiriwa Nabii Muhammad s.a.w. katika vitabu vya Kikristo na Kiyahudi, tazama: Kumbukumbu la Torati 18.19-22, na Injili ya Yohana 16.5-14.)