Skip to content
الأنعَام /

Aya 112

6 : 112

Aya 112 of الأنعَام (6 : 112). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 112

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوّٗا شَيَٰطِينَ ٱلۡإِنسِ وَٱلۡجِنِّ يُوحِي بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ زُخۡرُفَ ٱلۡقَوۡلِ غُرُورٗاۚ وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُۖ فَذَرۡهُمۡ وَمَا يَفۡتَرُونَ

Na kadhaalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashet'ani wa kiwatu, na kijini, wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba-pamba, kwa udanganyifu. Na angeli penda Mola wako Mlezi wasingeli fanya hayo. Basi waache na wanayo yazua.

Explanation & meanings · 1
  1. Kama ilivyo kuwa hao wamekufanyia uadui na inadi, na hali wewe unataka kuwaongoa, basi kadhaalika tumemfanyia kila Nabii anaye peleka ujumbe wetu, maadui katika wanaadamu majeuri na majini majeuri, ambao wanajificha kwako na huwaoni, wakitiliana wasiwasi kwa maneno ya kupamba-pamba na udanganyifu, yasiyo na ukweli. Basi kwa hayo huingiza ghururi kwa uwongo! Na hayo yote ni kwa kudra ya Mwenyezi Mungu na kutaka kwake. Na lau angeli taka wasingeli fanya hayo. Lakini hayo ni kwa ajili ya kuzisafisha nyoyo za Waumini. Basi waachilie mbali hao walio potea na kufuru zao za maneno yao wanayo yazua.