Skip to content
الأنعَام /

Aya 111

6 : 111

Aya 111 of الأنعَام (6 : 111). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 111

۞ وَلَوۡ أَنَّنَا نَزَّلۡنَآ إِلَيۡهِمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَحَشَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ كُلَّ شَيۡءٖ قُبُلٗا مَّا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُوٓاْ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ يَجۡهَلُونَ

NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao wamo ujingani.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika hao walio apa kuwa ikiwajia Ishara wataiamini, ni waongo. Mwenyezi Mungu anaijua vilivyo imani yao. Lau kuwa sisi tungeli teremsha Malaika wakawaona kwa macho, na maiti wakawasemeza baada ya kufufuliwa makaburini mwao, na kuwakusanyia kila kitu mbele yao kikiwakabili na kuwabainishia haki, bado wasingeli amini ila akipenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa waamini. Na wengi hawaitambui Haki wala hawaifuati, kwa sababu nyoyo zao zimesibiwa na upofu wa kijahiliya.