Skip to content
البَقَرَة /

Aya 239

2 : 239

Aya 239 of البَقَرَة (2 : 239). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 239

فَإِنۡ خِفۡتُمۡ فَرِجَالًا أَوۡ رُكۡبَانٗاۖ فَإِذَآ أَمِنتُمۡ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ

Ikiwa mnakhofu (Salini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapo kuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu kama alivyo kufunzeni yale mliyo kuwa hamyajui.

Explanation & meanings · 1
  1. Ukikufikieni wakati wa Swala nanyi mko katika khofu basi msiache kusali, bali swalini kama muwezavyo, ikiwa huku mnakwenda kwa miguu au mmepanda kipando. Ikiondoka khofu swalini kwa kutimiza nguzo zote kama mlivyo jifunza, mkimkumbuka Mwenyezi Mungu katika Swala na mkimshukuru kwa aliyo kufunzeni, na kwa kukujaalieni kuwa katika amani.