Skip to content
البَقَرَة /

Aya 224

2 : 224

Aya 224 of البَقَرَة (2 : 224). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 224

وَلَا تَجۡعَلُواْ ٱللَّهَ عُرۡضَةٗ لِّأَيۡمَٰنِكُمۡ أَن تَبَرُّواْ وَتَتَّقُواْ وَتُصۡلِحُواْ بَيۡنَ ٱلنَّاسِۚ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Wala msifanye jina la Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa ni kisingizio cha kuacha kufanya wema na kuchamngu na kupatanisha baina ya watu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua.

Explanation & meanings · 1
  1. Msilichezee jina la Mwenyezi Mungu katika kukithirisha viapo, kwani hivyo inakuwa ni kinyume na kulitukuza jina la Mwenyezi Mungu. Na hakika kujilinda na kukithirisha kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ndio hupelekea vitendo vyema, na kuchamngu, na kuweza kusuluhisha baina ya watu. Mwenye kujilinda hivyo huwa anatukuka cheo katika macho ya watu, na anakuwa anaaminika, na kauli yake hukubalika kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maneno yenu na yamini zenu, na Mjuzi wa niya zenu.