Skip to content
البَقَرَة /

Aya 225

2 : 225

Aya 225 of البَقَرَة (2 : 225). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 225

لَّا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغۡوِ فِيٓ أَيۡمَٰنِكُمۡ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتۡ قُلُوبُكُمۡۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi. Bali anakushikeni kwa yanayo chuma nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu amekusameheni baadhi ya yamini (viapo) zenu. Lilio mpitia mtu ulimini mwake katika viapo bila ya kukusudia wala kulitia moyoni, au akaapa kwa kuamini kuwa limetukia na halikutukia, Mwenyezi Mungu hayachukulii hayo. Lakini anakushikeni kwa mnayo yaazimia katika nyoyo zenu kuwa yamekuwa au hayakuwa, na kwa kusema uwongo pamoja na kuuwapia yamini. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumghufiria mwenye kutubu, ni Mpole, anasamehe lisilo kusudiwa moyoni.