Skip to content
Al-Baqarah /

Aya 216

2 : 216

Aya 216 of Al-Baqarah (2 : 216). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Baqarah Aya 286
Sura · Al-Baqarah
Kiswahili · Barawani
2 : 216

كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ وَهُوَ كُرۡهٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ شَرّٞ لَّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.

Explanation & meanings · 1
  1. Ikiwa kutoa kusaidia mayatima na masikini na wengineo ni kuhami jamii ya umma kwa ndani, kadhaalika kupigana vita ni kuuhami umma na adui wa nje. Kwa hivyo enyi Waislamu, mmelazimishwa kupigana vita kuhami Dini yenu, na kulinda nafsi zenu. Hakika hizo nafsi zenu kwa mujibu wa tabia zake zinachukia mno kupigana. Lakini huenda mkachukia kitu na ndani yake ipo kheri kwenu, na mkapenda kitu na ikawa ipo shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua maslaha yenu ambayo yamefichikana, na nyinyi hamyajui. Basi tendeni mlilo amrishwa kulitenda.