Skip to content
البَقَرَة /

Aya 215

2 : 215

Aya 215 of البَقَرَة (2 : 215). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 215

يَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَۖ قُلۡ مَآ أَنفَقۡتُم مِّنۡ خَيۡرٖ فَلِلۡوَٰلِدَيۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِينَ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِۗ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٞ

Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua.

Explanation & meanings · 1
  1. Waumini wanakuuliza mas-ala ya kutoa. Waambie: Kutoa iwe kutokana na mali mazuri, na wa kupewa ni wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri aliye katikiwa na mali yake na watu wake. Na lolote katika vitendo vya kheri mlitendalo basi hakika Mwnyezi Mungu analijua na atakulipeni kwalo.