Skip to content
هُود /

Aya 1

11 : 1

Aya 1 of هُود (11 : 1). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 1

الٓرۚ كِتَٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ

Alif Lam Ra. Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimewekwa wazi, kisha zikapambanuliwa, kilicho toka kwa Mwenye Hikima na Mwenye Khabari!

Explanation & meanings · 1
  1. Alif Lam Ra (A.L.R.)...Hizi ni harufi zilizo anziwa Sura hii kuwa ni ishara kuwa Qur'ani ni muujiza juu ya kuwa imeundwa kwa hizi hizi harufi zinazo tamkwa, na pia ni kuwazindua watu wanapo isikiliza inapo somwa Qur'ani Tukufu kuwa ni Kitabu chenye shani kuu. Zimeteremshwa Aya zake zimeshikana, madhubuti, hazina ndani yake upotovu, wala ubabaishi, na zimetungwa kwa njia isiyo na dosari, iwazi, na yenye kubainisha. Kisha hukumu zake zikapambanuliwa. Na Kitabu hichi juu ya utukufu wake ulio nao nafsi yake, kina utukufu zaidi kwa kuwa kimetokana na Mwenyezi Mungu ambaye anajua kila kitu, na Yeye Subhanahu anapanga mambo yote kwa pahala pake.