Skip to content

Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kuamini siku ya mwisho?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: vipi inakuwa kuamini siku ya mwisho?

الجواب

Jawabu/ sema: Ninaamini kwa mkato na yakini isiyokowa na shaka ndani yake na nikiwa ni mwenye kukiri kutokea yote aliyo yaeleza Mwenyezi Mungu kuhusu kutokea kwake baada ya kufa, ikiwemo kuulizwa maswali kaburini na neema za kaburini na adhabu zake na kufufuliwa na kukusanywa viumbe kwa ajili ya kuhesabiwa na kuhukumiwa na yale yatakayo kuwa katika uwanja wa kufufuliwa, ikiwemo kisimamo kirefu na jua kusogea kiasi cha maili moja na hawdhwi (Bwawa) na mizani na kupewa vitabu vya matendo ya waja na kuwekwa njia ambayo itakuwa juu ya moto wa Jahanam na mengineyo miongoni mwa matukio na vitisho vya siku hiyo kubwa, mpaka watu wa peponi waingie peponi na watu wa motoni waingie Motoni, kama ilivyo elezwa kwa uwazi katika Qur'an na sunnah za Mtume rehma na amani ziwe juu yake na inaingia katika imani ya kuamini siku ya mwisho, kusadikisha yale yalio thibiti katika alama za Qiyama na alama zake ikiwemo fitina kukithiri, kuuwana , matetemeko na kudidimizwa ardhini,na kutoka Dajali na kushuka kwa nabii Issa amani ziwe juu yake na kutoka kwa Yaajuju na Maajuju na kuchomoza jua kutoka katika upande wa Magharibi na alama zinginezo miongoni mwa alama za Qiyama.

Na zote hizo zimethibiti katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na habari za Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake zilizo sahihi zilizo andikwa katika vitabu vya Hadithi sahihi.